Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Picha za viatu na koti vinavyodaiwa kuwa vya Kiongozi Shahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Ali Khamenei, zimevutia hisia za wengi katika mitandao ya kijamii, huku zikitajwa kuwa mfano wa maisha yake ya unyenyekevu na kutokuwa na shauku ya anasa za dunia.
Wanaounga mkono mtazamo huo wanasema kuwa, licha ya kuiongoza nchi iliyojenga uwezo mkubwa katika sekta mbalimbali za kilimo na viwanda na kusimama dhidi ya mataifa yenye nguvu duniani, Khamenei aliendelea kuishi maisha ya kawaida yanayofanana na ya wananchi wa kawaida.
Picha hizo zimeendelea kujadiliwa kama ishara ya mtindo wake wa maisha, huku zikichochea maoni tofauti miongoni mwa wachambuzi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu urithi wake wa kisiasa na kijamii.

Shahidi Sayyid Ali Khamenei alitumia maisha yake yote kwa mujibu wa ujumbe huu akiwatumikia watu wake.
1_Hakuwahi kutanguliza tamaa ya kujinufaisha binafsi.
2_Hakuhusika na udanganyifu au uchezeshaji wa masoko kwa maslahi yake.
🚩3_Hakuhusika na uporaji wa rasilimali za mafuta za mataifa mengine.
🏴4_Hakuhusika na utekaji wa viongozi wa mataifa ya kigeni.
5_Hakubadilisha misimamo yake mara kwa mara kwa maslahi ya kisiasa.
6_Hakushambulia mataifa mengine.
Your Comment